Ads

HUYU HAPA RICKY REGUFE NA NDIO KILA KITU KWA RONALDO(CR7)........


Wengi wanaweza kuwa wanamfahamu na kufurahishwa na kazi ya wakala Jorge Mendes katika kila linapokuja suala la biashara za wateja wake kwani ni wakala wa wachezaji na makocha maarufu duniani kuanzia kwa Cristiano Ronaldo mpaka kwa Jose Mourinho.
Lakini pamoja na hayo yote nyuma ya pazia kuna watu mashuhuri ambao wamekuwa wakichangia maendeleo na mafanikio ya watu hawa maarufu huku pia wakiwa ndio watu wanaowapa ushauri wanaouamini kuliko kitu chochote kile. Mmoja wa watu hawa ni mwanaume mmoja anayeitwa Ricky Regufe.
Ricky ni mmoja kati ya meneja masoko wa kampuni ya Nike maarufu kabisa. Lakini kazi yake ndani ya Nike haikuja hivi hivi, aliitafuta, aliipigania na akaipata na leo anakula bata.
Cristiano Ronaldo embraces Ricky Regufe after Portugal's victory over Wales at Euro 2016
Ricky alikuwa moja ya wachezaji vijana ambao walikuwa wanatamani kuja kuwa wachezaji bora baadae. Lakini alipoona soka sio sehemu yake aliamua kustaafu akiwa na umri wa miaka 21 tu. Aliamua kustaafu ili abobee kwenye masuala ya kusimamia masoko ya wanamichezo.
Miaka michache baadae akakutana na kijana mwenye kipaji cha aina yake akiwa Sporting Lisbon, jina lake ni Cristiano Ronaldo. Ricky akuhitaji saini yake, akuhitaji urafiki wake na wala kuwajua marafiki zake Ronaldo na hivi walikuwa na tofauti ya miaka 6 tu.
Alichokifanya Ricky ni kuhakikisha Ronaldo anashawishika kujiunga na kuwa chini ya usimamizi wa kampuni ya vifaa vya michezo ya Nike. Hili ndilo lilikuwa dhumuni lake kubwa na ambalo lilifanikiwa na ambalo Nike hawataki kumsahau mtu huyu, pengine wanampenda kuliko hata Ronaldo mwenyewe kwani ndiye chanzo cha utajiri wao kupitia Ronaldo.
The two men, pictured playing poker, have known each other for the past 13 years
Nike walimchukua awe mtu wao wa kuwatafutia mastaa wa Ureno kwa ajili ya kupata saini zao za udhamini wa vifaa vya michezo na Ricky hakuwaangusha waajiri wake. Pengine bila yeye, Nike wasingekuwa naye Ronaldo huyu.
Ndiyo yeye aliyeweza kumnyanyua kijana mdogo aliyekuwa anajua kukimbia katika eneo la winga, akiwa katengeneza nywele zake na kumueleza umuhimu wa miguu yake kumuingizia mamilioni nje ya mshahara wake. Huyoo akaokota dodo lake na sasa limeiva.
Mpaka sasa imekuwa ni miaka 13 ya ukaribu wao kiasi cha watu wanaowafahamu kuamua kuunganisha majina yao na kuwa CRICKY. Ni zaidi ya ndugu, zaidi ya marafiki na sasa Ricky ndiye mtu pekee ambaye anaweza kumshauri Ronaldo, kumfanyia maamuzi ya kibiashara na pia kuwa mtunza siri wa maisha binafsi ya Ronaldo.
Ronaldo was a youngster in the Sporting Lisbon set-up when he was spotted by Regufe
Mpaka leo, nje ya mishahara ambayo inatokana na kipaji chake ndani ya uwanja, Ronaldo amefikia hatua anavuna kiasi cha zaidi ya paundi milioni 14 kwa mwaka, kupitia mikataba ya kibiashara inayotakana na binadamu huyu.
Pengine Ronaldo anamwamini zaidi kutokana na tabia yake ya usiri. Mpaka leo hii hakuna chombo cha habari kilichowahi kufanikiwa kumuhoji Ricky na mara zote amekuwa akikwepa hili, hivyo kazi yake ni simu za biashara na kalamu kwa ajili ya mikataba ya Ronaldo wake.
Refuge (centre) is often pictured on the Real Madrid players' social media pages
Amekuwa ni sehemu ya maisha ya Ronaldo kwa sasa kuliko hata ilivyokuwa Nike na muda wote wako wote na wanakula bata wote. Cristiano Ronaldo hachoki kumweka kwenye mitandao yake ya kijamii na huwezi kumkosa katika matukio ya kifamilia ya Ronaldo pengine kuliko hata mama yake mzazi.
Ameonekana mara kadhaa akiwa katika mazungumzo na wadada maarufu duniani kama Jenifer Lopez, Kim Kardashian na wengine wengi na umaarufu huu kwa mastaa wakubwa unatokana na mchezaji huyu.
Ndio maana pia sio jambo la ajabu kuona kuwa katika miezi minne iliyopita, Ricky ameambatana na Ronaldo katika matamasha kama tuzo cha mchezaji bora wa Ulaya, kombe la mataifa ya Ulaya, mapumzikoni Marekani ambapo aliambatana na mpenzi wake Claudia Dinis.
Regufe's girlfriend, fashion blogger Claudia Dinis, poses with him in matching Ronaldo shirts
Hii ilipelekea hata chama cha soka cha Ureno kuamua kumpa utambuzi rasmi (accreditation) ili aweze kuungana na timu yao ya Taifa katika mashindano ya mataifa ya Ulaya hivyo kuwa miongoni mwa watu waliokuwa kwenye msafara wa timu hiyo.
Hii yote ni katika kutambua umuhimu wa mtu huyu katika maisha ya Cristiano Ronaldo. Huyu ndiye nguzo yake na ndiye ambaye anaamua maisha yake kwa kiasi kikubwa kuliko hata Cristiano Ronaldo yeye mwenyewe.
Ndio maana haikuwa ajabu kamera kuwanasa watu hawa wakifurahia kwa hisia kubwa baada ya Ureno kutwaa taji baada ya kuwafunga Ufaransa kwa goli la dakika za nyongeza. Walifurahi pamoja, walitoa machozi ya furaha kwa pamoja na walishinda kwa pamoja.
He was quick to congratulate Ronaldo after Portugal beat Poland on penalties at Euro 2016
There were similar scenes after Portugal beat France 1-0 in the European Championship final
TV cameras filmed the pair in an emotional embrace after the end of the match
Watu wengi wanaweza kuwa wanajiuliza juu ya chapa ya CR7. Ukweli ni kuwa tofauti na wengi ambao chapa zao zipo chini ya mawakala, ya Ronaldo ipo chini ya mtu huyu ambaye pia ndiye rafiki yake kipenzi. Huyu anahakikisha mikataba minono inamwagika kila kukicha.
Ifuatayo ni orodha ya udhamini ambao ameifanikisha kwa Ronaldo na kisha ujue umuhimu wake, na undugu wake. Anaitwa Ricardo Regufe na sio Jorge Mendez.
Biashara: CR7 underwear, CR7 footwear, Legacy (manukato), CR7 shirts, Pestana Hotels, CR7 Museum
Udhamini: Nike, Tag Heuer, Sacoor Brothers, Monster headphones, PokerStars, HerbalLife, Clear, Xtrade
Ubalozi na hisani: Save The Children, Abbott (blood and plasma donation)
Follow Insta @nicasiusagwanda

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.