Ads

Huwezi kuamini Tunzo za Kilimanjaro zimempoteza 20%........

Image result for msanii 20 percent



Haya sasa hivi nikwanini waliamua kusema ukiona kobe kainama basi ujue anatunga sheria? na haikuishia hapo wakasema tena aliyeko juu msubirie chini mana ipo siku atashuka tu.Nikiwa najiuliza yote haya nikajikuta napata majiku kupitia kwa huyu jamaa ambaye wengi kwa kitendo cha kuchukua tunzo tano kiliwashangaza kweli.

       Hebu leo tuanze safari ya kujua yeye ninani, ana nini, na nikwanini.Jamaa mwenye sio mwingine ni mwanamziki 20% ama unaweza kumuita Abbas Hamis Kisanza.20 ni moja ya wasanii wenye mafanikio makubwa ya muziki wa hapa nchini Tanzania na wengineo kama Jpseph Haule,Ispector Haroon, Juma Kasim(nature), Afande Sele na wengine wengi.

20% ni jamaa mmoja mcheshi sana na ni baba na anaishi na mke wake hapa jijini Dar es Salaam Kimanzichana, Wilaya ya Mkuranga, Mkoa wa Pwani.Kwaujumla 20% kwao wamezaliwa watoto 20 kwakuwa baba yao ambeye nimarehemu kwa sasa alikuwa ameoa wanawake wengi na kwa upande wa mama yake wamezaliwa watoto tisa.

      20% licha ya kuwa msanii bora na kutwaa tunzo tano kwampigo kwenye tunzo zaKilimanjaro Music award pia nimoja ya waigizaji wazuri wafilamu hapa nchini na kudhihirisha hilo PER ana kituo chake cha sanaa ya maigizo kinachojulikana kwa jina la "SIMBA MWEUPE"(White lion).


       Sitaki nikuchoshe leo tuangalie japo PER yupo kimya lakini ni kwanini nyimbo zake hazichuji

Utajiliza kwanini jamaa yupo kimya tangu achukue tunzo, haonyeshi upinzani wowote, humsikii hata kwenye Interviewas kwenye vituo vya radio na Televion lakini bado nyimbo zake hazichuji ukweli nihuu hapa, ukisikiliza nyimbo zake kama vile Money money, Bange, Yanini malumbano, Maisha ya bongo, Nema, Binti kimanzi, na nyinginezo nyingi utagudua kitu kuwa 20% ana kitu adhwiimu kutoka kwa mungu.Nacho si kingine bali niubunifu wa hali ya juu alionao PER kwakuimba mambo yaliyopo na sio yakufkiria tena yakiwa yaniguza nchi ya tanzania.


   Lakini sasa ona mungu alivyo mtu waajabu baada ya PER kutwaa tunzo hizo ndipo balaa lilipoanzia kwani ndio ilikuwa mwanzo wa jamaa kushuka kiwango na kupotea kwenye mziki wa bongo flava japo kutokana na umaarufu alionao watu wanaamini akitoa nyimbo itakubalika.

 Sasa nikwanini mtu kapata tuzo zenye thamani ya juu alafu ziwe chanzo cha yeye kupotea katika kazi hiyohiyo ambayo imempa tumzo hizo? nitakuambia kesho wewe endelea kutembelea blog   24 hours blog.



      

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.