Ads

Airlander 10: Ndege ndefu zaidi duniani yapata ajali......

 ndefu zaidi duniani - Airlander 10 - imeharibika baada ya kuanguka ikitua kwenye safari yake ya pili ya kufanyiwa majaribio.
Ndege hiyo ya urefu wa 302ft (92m) - ambayo kwa kiasi fulani ni ndege na pia kwa kiasi fulani puto - iliharibika ikiwa katika uwanja wa Cardington, Bedfordshire nchini Uingereza.
Ndege hiyo ya thamani ya £25m imeharibika eneo wanamoketi marubani baada ya kuangika kwa 'pua' mwendo wa saa tano saa za Uingereza.
Msemaji wa HAV, kampuni iliyounda ndege hiyo, amesema marubani na wahudumu wengine wote wako salama.
Kampuni hiyo imekanusha madai kwamba waya uliokuwa umening'inia kutoka kwenye ndege hiyo ulikwama kwenye kigingi cha nyaya za simu na kusababisha ajali hiyo.
Ndege hiyo ilifanya safari yake ya kwanza 17 Agosti.
AirlanderImage copyrightSBNA
Image captionNdege hiyo imeharibika sehemu wanamoketi marubaniage caption
Kampuni ya HAV inapanga kuunda ndege 10 aina ya Airlander kufikia mwaka 2021.
Airlander 10Image copyrightSBNA
Image captionHAV inapanga kuunda ndege 10 za Airlander kufikia mwaka 2021

Airlander 10 kwa takwimu
  • 44,100 lbs (20,000kg): Uzani wa ndege hiyo
  • 20,000ft (6,100m): Umbali ambao inaweza kupaa juu angani
  • 80 knots (148km/h): Kasi yake ya juu zaidi
  • Siku 5: Muda ambao inaweza kukaa angani
  • 22,050 lbs (10,000kg): Uzani ambao inaweza kubeba

AirlanderImage copyrightSOUTH BEDS NEWS AGENCY
Image captionNdege hiyo imeharibika eneo wanamoketi marubani

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.