Ads

Maneno mazito Lissu alomwambia Zito!!!





KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amerejea nchini akitokea Nairobi, Kenya alikokwenda mwishoni mwa wiki kumjulia hali Tundu Lissu na akitaja maneno mawili aliyodai kuambiwa na Mwanasheria huyo Mkuu wa Chadema jijini humo.


zitto alikwenda Nairobi Jumamosi kufuatilia maendeleo ya kiafya ya Mbunge huyo wa Singida Mashariki (Chadema) ambaye anapatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Nairobi baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana nyumbani kwake Area D mjini Dodooma Septemba 7.

Katika kurasa zake za mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter jana, Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini alitaja maneno mawili aliyodai kuambiwa na Lissu hospitalini huku akieleza kuwa Rais huyo wa Chama cha Wanasheria (TLS) ni jasiri.

"Nimetumia wiki-endi iliyopita kumsabahi ndugu Tundu Lissu mjini Nairobi, nimerudi nikiwa mwenye unyeyekevu zaidi kwa sababu ya nguvu na ujasiri ambao kaka yangu ameuonyesha licha ya kuwa kwenye maumivu makali," Zitto alieleza.

"Si mara nyingi hapa nchini utasikia kukiongelea ujasiri, lakini namfikiria Lissu na vile nilivyojisikia nikiwa pamoja naye Nairobi.

"Najua hivyo ndivyo alivyo. Waliomshambulia wamemuumiza. Wamemuumiza kweli. Na bado wakati tuliokuwa naye amenionyesha shukrani, ari na pia ucheshi. Huo ni ujasiri.

"Alichokipata na anachoendelea kukipata Lissu sio kitu rahisi kwa mtu yeyote kutafakari. Kufikiria hali ile kungeniacha nimeumia moyo sana kama asingesema maneno haya kwangu 'tumeshinda, tumeshashinda'. Ujasiri ni Lissu."

Baada ya kupigwa risasi, Lissu aliwahishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma alikopatiwa matibabu ya awali kabla ya kupelekwa Kenya usiku wa manane kwa ajili ya matibabu zaidi.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.