HAPATOSHI SIMBA NA YANGA NGAO YA HISANI
Dar es Salaam. Presha inapanda presha inashuka kila kona ya nchi kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii utaokaofanyika Jumatano ijayo Agosti 23, kati Yanga dhidi ya Simba.
Hii ni mara ya kwanza kwa Yanga na Simba kucheza mechi ufunguzi wa msimu tangu 2011 zilipokutana kwa mara ya mwisho katika mechi hiyo ya Ngao ya Jamii.
Katika mchezo huo wa Agosti 17, 2011, Simba ilishinda kwa mabao 2-0 magoli yaliyofungwa na Haruna Moshi ‘Boban’ na Mzambia Felix Sunzu.
Pamoja na ushindi huo Yanga ndiyo yenye rekodi nzuri ikiwa imeifunga Simba mara mbili na kufungwa mara moja kabla ya mechi ya Jumatano ijayo.
Yanga ilifunga Simba katika mechi ya ufunguzi wa mashindano hayo mwaka 2001 kwa mabao 2-1. Katika mchezo huo mabao ya Yanga yalifunga na Edibily Lunyamila na Ally Yusuph ‘Tigana’ wakati lile la Simba lilifungwa na Steven Mapunda ‘ Garincha’.
Yanga ilifunga tena Simba kwa penalti 3-1 baada ya kumaliza kwa suluhu mwaka 2010.
Kihistoria ya mashindano hayo yanaonyesha Yanga imeshiriki mara nyinyi zaidi saba ikitwaa ubingwa mara tano ikifuatiwa na Simba iliyoshiriki mara tano ikitwaa ubingwa mara mbili.
Azam imeshiriki mara tano na kutwaa ubingwa mara moja wakati Mtibwa Sugar imecheza mara moja 2009 ilicheza na Yanga baada ya Simba kugoma. Mtibwa ikashinda mabao 2-1 na kutwaa Ngao hiyo.
Mabingwa wa Ngao ya Jamii
Mwaka Mshindi Matokeo
2001 Yanga 2-1 Simba
2009 Mtibwa Sugar 2-1 Yanga
2010 Yanga 0-0 Simba (3-1penalti)
2011 Simba 2-0 Yanga
2012 Simba 3-2 Azam
2013 Yanga 1-0 Azam
2014 Azam 0-3 Yanga
2015 Yanga 0-0 Azam (penalti 8-7)
2016 Azam 2-2 Yanga (4-1 Penalti)
2017 Yanga v Simba
No comments