SINGIDA UNITED WATUMA MESSAGE KWA YANGA NA SIMBA...
Wachezaji wa kikosi cha Singida United wameahidi kuleta ushindani msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania bara 2017/2018.
Kikosi hicho chenye maskani yake mkoani Singida chini ya kocha wake mkuu, Hans Pluijm kimejipatia umaarufu mkubwa kutokana na usajili walioufanya kwa kuwanasa wachezaji kadhaa wa kigeni.
Nizar Khalfan ambaye ni nahodha wa kikosi hicho amesema nia yao ni kufanya kweli katika msimu huo mpya wa Ligi ambao utafunguliwa kwa mchezo baina ya Simba na Yanga.
“Tumekuwa na mipango yetu kama timu ambayo tunahitaji kuifanikisha, uzuri kila mmoja wetu anaonekana kuwa na hali ya kutaka kufanya vizuri nafikiri hatutowaangusha pia mashabiki zetu.” alisema Nizar.
Naye Kiungo wa Kenny Ally ambaye ametua kwenye timu hiyo akitokea Mbeya City amesema watu wasubiri vitu vizuri kutoka kwao maana wanajipanga kufanya vizuri.
No comments