Ads

BUSUNGU AKIPATA MILIONI 10 YANGA ANDIKENI MAUMIVU...


Image result for busungu

Malimi Busungu hajacheza mechi za ushindani karibu mwaka sasa zaidi ya kufanya mazoezi pekee, lakini Lipuli FC ambao wamepanda daraja wanahitaji huduma yake ila kumpata ndiyo bado kumekuwepo na ugumu kwani anahitaji dau la Sh10 milioni ya usajili.
Lipuli imepanda daraja kushiriki Ligi Kuu msimu ujao na ni timu ambayo mpaka sasa inafanya usajili kwa mafungu kutokana na ukata unaowakabili na ndiyo maana bado wanafanya mazungumzo na Busungu ili japo ashuke kidogo.
Meneja wa mchezaji huyo, Yahya Tastao alisema wanaamini mazungumzo yao yatafikia mwisho kwani hata wao nia ni mchezaji wao acheze ili arejee kwenye kiwango chake cha zamani.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.