TETESI ZA SOKA ULAYA LEO IJUMAA 30...
Arsenal wamejitoa katika mbio za kumwania nyota wa Monaco Kylian Mbappe, 18, na sasa wataelekeza nguvu zao kumpata Alexandre Lacazette na Thomas Lemar (Mail Online).
Mesut Ozil ameonesha dalili za kubakia Arsenal baada ya kulipia tena chumba maalum cha kutazamia mpira (executive box) ndani ya uwanja wa Emirates (The Sun).
Antonio Conte hajafurahishwa na hatua ya Chelsea kumfuatilia Romelu Lukaku badala ya Andrea Belotti. Conte ameghadhibishwa kwa sababu wachezaji hao wawili bei yao ni moja, takriban pauni milioni 85, lakini mkurugenzi wa ufundi wa Chelsea Michael Emenalo ameamua kumfuatilia Lukaku badala ya Belotti (Daily Star).
Guangzhou Evergrande hawana mpango wowote wa kumuuza Paulinho kwenda Barcelona (Nanfang Daily).
Liverpool wapo tayari kupanda dau la pauni milioni 70 kumtaka kiungo wa kimataifa wa Guinea Naby Keita, 22 anayeichezea RB Leipzig (Mirror).
Liverpool wanataka kuwasajili Naby Keita pamoja na Alex Oxlade-Chamberlain, 23 (Liverpool Echo).
Liverpool wanataka kumsajili beki wa kushoto Andrew Robertson kutoka Hull City (Liverpool Echo).
Real Madrid huenda wakamsajili Eden Hazard, 26, kutoka Chelsea na Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco (Diario Madrista).
Everton watakamilisha usajili wa mshambuliaji wa Malaga, Sandro, 21, wiki ijayo (Liverpool Echo).
Alvaro Morata amewaambia marafiki wake kuwa ameamua kujiunga na Manchester United na kuwa mkataba tayari "umekamilika" (Daily Express).
Manchester United hawatomuuza Ander Herera kwenda Barcelona, licha ya taarifa kusema Barca watafikiria kumchukua iwapo watamkosa Marco Verratti, 24, kutoka PSG (Independent).
Barcelona wanamtaka Ander Herera na Riyad Mahrez, kama watashindwa kumsajili Marco Verratti (Sport.es).
Radja Nainggolan anayesakwa na Manchester United, huenda akajiunga na Inter Milan, baada ya klabu hiyo ya Italia kutoa dau la euro milioni 60 (101 Great Goals).
Jose Mourinho anafikiria kumchukua kiungo wa Middlesbrough Marten de Roon katika wiki chache zijazo (TuttoMercatoWeb).
Manchester City wameanza mazungumzo na Tottenham kuhusiana na beki wa kulia Kyle Walker, lakini Spurs hawataki kupokea chochote chini ya pauni milioni 50 (The Mirror).
Manchester City huenda wakaamua kumfuatilia winga wa Bayern Munich Kinglesy Coman (RMC).
Chelsea wanafikiria kumfuatilia beki wa Roma, Kostas Minolas, 26, ambaye alikuwa anakaribia kujiunga na Zenith St Petersburg kwa pauni milioni 26 (London Evening Standard).
Meneja wa Chelsea Antonio Conte anaghadhibishwa na jinsi klabu yake inavyoendesha shughuli za usajili (Star).
Real Madrid bado wanamtaka mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, licha ya klabu hiyo kusema haina mpango wa kumuuza mchezaji huyo kutoka Ubelgiji (OK Diario).
Chelsea wanajiandaa kutaka kupanda dau kwa beki wa Bayern Munich Jerome Boateng (Daily Mirror).
Chelsea wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa PSG katika kumsajili beki wa Juventus Alex Sandro (The Mirror).
Southampton wanamtaka mshambuliaji wa Manchester City Kelechi Iheanacho, 20 ambaye thamani yake ni pauni milioni 25 (Sun).
Meneja wa Watfrod Marco Silva amedhamiria kumsajili Kieran Gibbs, 27, kutoka Arsenal. Beki huyo pia amehusishwa na kuhamia Liverpool (Mirror).
Monaco hawatarajii kumuuza Thomas Lemar, 21, msimu huu, na wamewaambia Arsenal na Tottenham kuwa mchezaji huyo hauzwi (Independent).
Licha ya tamko hilo, Barcelona nao wamesema wanamtaka Thomas Lemar (L'Equipe).
Mshamnuliaji wa zamani wa Arsenal na Manchester United Robin van Persie huenda akarejea katika EPL msimu ujao na kujiunga na Crystal Palace (Daily Mirror).
Meneja mpya wa Nantes, Claudio Ranieri anamtaka kipa wa Arsenal David Ospina (France Football).
Meneja wa Brighton Chris Hughton amethibitisha kuwa klabu yake imewasiliana na Liverpool kuhusu kumsajili beki Joe Gomes, 20 (Brighton Argus).
Beki wa Hull City Andy Robertson, 23, anasakwa na Liverpool, kwa sababu Jurgen Klopp anataka kusajili beki mpya wa kushoto (Liverpool Echo).
Rais wa Bayern Munich Uli Hoeness amesema hawatomsajili Alexis Sanchez, 28, kutoka Arsenal, kwa kuwa klabu yake inazingatia kusajili wachezaji chipukizi (Kicker).
Mtoto wa Zinedine Zidane, Enzo, 22, ameondoka Real Madrid na kujiunga na Alves kwa kusaini mkataba wa miaka mitatu, baada ya kukosa namba katika timu inayofundishwa na baba yake (FourFourTwo)
Kiungo Saul Niguez, 22, anataka kubakia Atletico Madrid, lakini huku Barcelona na Manchester United zikimtaka, anasema angependa kupata pesa zaidi (Goal).
Mwenyekiti wa West ham David Gold amesema hawamfuatilii Jack Wilshere, 25, lakini klabu yake inatafuta washambuliaji wawili wapya na wenye uzoefu wa EPL (TalkSport).
Newcastle wanakaribia kumsajili beki wa Eibar, Florian Lejeune, 26, na pia wanataka kumshawishi Andre Gray, 26 kutoka Burnley (Newcastle Chronicle).
Na hatimaye…..
Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameonesha picha ya mapacha wake na kusema "Nina furaha sana ya kuweza kuwabeba wapenzi wangu wapya katika maisha yangu".
Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa.
Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii (kwa Kiingereza): Wachezaji waliokamilisha usajili
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Siku njema.
No comments