Kocha wa Lesotho afurahia sare na Tanzania...
Kocha wa timu ya taifa ya Lesotho Moses Maliehe amesema kupata sare ugenini ni matokeo bora kwao ukizingatia walikuwa wanapambana na timu yenye uwezo mkubwa.
Matokeo ya sare kwa upande wetu ni mazuri kwa sababu unapocheza mechi ugenini hutakiwi kushambulia mwanzo mwisho kwa timu kama Tanzania kwa sababu wana kasi na kama nilivyotangulia kusema mwanzo Tanzania ni timu nzuri.
“Tunafurahi kupata sare ugenini na tumecheza kama tulivyopanga awali dhidi ya Tanzania, sare ni matokeo bora sana kwetu.”
Maliehe amesema walikuja wakiwa na lengo la kushinda lakini kutokana na ubora uliooneshwa na Stars hawakufanikiwa kupata ushindi badala yake wakaambulia sare ya kufungana bao 1-1.
“Tulijipanga kushinda lakini haikuwezekana kwa sababu tumecheza na timu nzuri (Tanzania) wanakimbia sana uwanjani .”
“Mchezo ulikuwa mgumu sana na tulitarajia hivyo kwa sababu tulikuwa tunacheza ugenini, ukiangalia wachezaji wangu walicheza kwa kujituma kwa dakika zote.”
Tanzania itajipanga tena kwa ajili ya mechi ya mwezi ujao dhidi ya Rwanda kuwania kufuzu michuano ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani maarufu kama CHAN.
No comments