Ads

Wenger afanya mazungumzo na Stan Kroenke juu ya mkataba mpya...

Kroenke (kulia) amewahi kumtaja Wenger kama kocha bora kwa klabu hiyo

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amefanya mkutano muhimu na mmliki wa klabu hiyo Stan Kroenke Jumatatu ambapo mustakabali wa mfaransa huyo ulitarajiwa kujadiliwa.
Matokeo ya mkutano huo bado hayajawekwa wazi, lakini maamuzi yanabaki baina ya Wenger na Kroenke na yatategemea pia kikao cha bodi kitakachojadili suala hilo leo hii.
Bado haijajulikana kama Wenger ataongeza mkataba baada ya kudumu katika klabu hiyo kwa miaka 21.
Masharti ya mkataba mpya yalikubaliwa miezi kadhaa iliyopita, lakini hakuna kilichofanyiwa kazi mpaka hivi sasa.
Ushindi wa kombe la FA siku ya jumamosi umekua faraja mpya kwa Wenger
Kumaliza pia nje ya timu nne bora na kukosa michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu ujao imekua changamoto kwake.
Idadi ya vikombe Wenger alivyofanikiwa kuvibeba akiwa Arsenal
Lakini hali kidogo imAekua shwari baada ya kuifunga Chelsea 2-1 katika fainali za kombe la FA siku ya Jumamosi na kumfanya Wenger kuwa kocha mwenye mafanikio zaidi kwenye kombe hilo huku Arsenal nayo ikiwa na mafanikio zaidi kuchukua kombe hilo.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.