Ads

Wanaume waliofumaniwa wakifanya mapenzi Indonesia kuchapwa viboko leo...........

Wanaume hao wa miaka 20 na 23 walifumaniwa wakiwa ndani ya kitanda na makundi ya sungusungu yaliyovamia makaazi yao mwezi machi.


Haki miliki ya picha

Wanaume wawili wanatarajiwa kupokea adhabu ya viboko katika mkoa wa Acheh nchini Indonesia baada ya kupatikana na hatia ya kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Indonesia imeharamisha mapenzi ya Jinsia moja na Mkoa wa Acheh hutawaliwa na sheria ya kidini- Sharia.
Wawili hao watapokea viboko 85 kila mmoja adhabu ikitolewa mbele ya umma.
Wanaume hao wa miaka 20 na 23 walifumaniwa wakiwa ndani ya kitanda na makundi ya sungusungu yaliyovamia makaazi yao mwezi machi.
Kabla ya kufumaniwa na kundi la sungu sungu mmoja wao alikuwa ni mwanafunzi wa chuo kikuu akisomea udaktari.

Mosque in Banda Aceh

Aliwaambia waandishi wa habari kuwa mipango yake ilikuw akuwe daktari. Kwa sasa inaripotiwa kuwa chuo alichokuwa akisomea kimemtimua.
Video za wawili hao wakifumania zilisambazwa kwa wingi kwenye mitandao ya kijamii wakiwa wote uchi huku wakiomba msaada.
Sheria kali dhidi ya mapenizi ya jinsia moja zilipitioshwa mwaka 2014 na kuanza kutekelezwa mwaka uliofuatia.
Hukumu za kuchapwa viboko zimetolewa awali kwa makosa yanahusu kucheza kamari na unywaji pombe.

Map

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.