UKISIKIA NYUMA GEUKA YAMEMKUTA HUYU NAYE..........................
Duniani tunajifunza na kuona vitu vingi tofauti vya kushangaza, kuogofya na kufurahisha,
Wengi wetu hatumjui Valentine Strasser ambaye aliwahi kuwa rais wa nchi ya Sierra Leone kati ya Aprili 29, 1992 hadi Januari 16 , 1996 akiwa ndiye amiri jeshi mkuu na kiongozi wa ngazi ya juu kwenye taifa hilo lililopo kaskazini-magharibi mwa bara la Afrika.
Wakati akiingia madarakani aliweka rekodi ya kuwa kiongozi mwenye umri mdogo zaidi, yaani akiwa na chini ya miaka 25.Kapteni Valentine Strasser kiongozi wa mapinduzi ya Rais Saidu Momoh.
ILIKUWAJE KUWAJE MAPAKA AKAWA RAIS MDOGO ZAIDI DUNIANI KWA WAKATI HUO?
Aprili 29, 1992, Strasser akiwa mwanajeshi kijana mwenye cheo cha kapteni, akiwa na umri wa miaka 25 tu, aliwaongoza wanajeshi wenzake kuvamia Ikulu ya Sierra Leone, walimkuta raisJoseph Saidu Momoh amejificha ndani ya kabati lililopo kwenye chumba cha kuogea, kisha wakamteka na wakamlazimisha kukimbia, naye akatorokea jijini Conakry nchini Guinea.
Baada ya mapinduzi kufanikiwa rais
Strasser alichukua madaraka ya nchi hiyo siku tatu tangu ashehereke sikukuu yake ya kuzaliwa na baada ya kuthibitika kwamba aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Momoh kutorokea Conakry, mwanajeshi Strasser alijitangaza kuwa rais wa Sierra Leone. Aliwaongoza vijana wenzake sita waliofanikisha mapinduzi hayo na kuunda serikali ya mpito waliyoipa jina la National Provisional Ruling Council (NPRC).
KAMA KAWAIDA MADARAKA YANALEVYA
Baada ya kuwa rais kamili,maisha yakabadilika kwakuwa tu ashakuwa mkuu wa nchi, kwa hiyo hakutaka kuishi kwenye nyoyo za wananchi wake Sierra Leone,Hakukumbuka tena kulipa malimbikizo ya mishahara ya wanajeshi na watumishi wengine wa umma,alifuja almasi ya Sierra Leone na rasilimali zingine na kupelekea kuchukiwa na wananchi na wanajeshi wenzake kwa mda mfupi,
Maajabu mengine ya bwana huyu
kwa vile jina lake ni Valentine, basi sikukuu ya Valentine’s Day ambayo dunia yote huazimisha kila ifikapo tarehe 14 ya mwezi 2,akaifanya kuwa sherehe hiyo kuwa miongoni mwa sherehe za kitaifa yenye mapumziko huku sherehe kubwa ikiandaliwa ikulu ya nchi hiyo na kula bata sana.
Bwana huyu alikuwa bingwa wa mbwembwe na starehe
Rais Strasser alikuwa mtu wa mbwembwe nyingi na kupenda sifa na kusifiwa,kwa mfano mwaka 1993 katika mkutano wa wakuu wa serikali katika nchi za Jumuiya ya Madola, uliofanyika Limassol nchini Cyprus, alitinga kwa mbwembwe akiwa amevaa suruali ya jeans na fulana yenye maandishi Sunny Days in Cyprus (Siku za Jua Kali Cyprus) ,kitu kilichokuwa kama dharau kwa waCyprus,alikuwa mtu wa starehe sana,mbabe, vurugu nyingi,na mpenda wanawake (womenizer),pia kipindi cha utawala wake aliua watu wasio na hatia,na hasa wapinzani wake.
Rais Strasser alisahau na kujisahau kuwa ipo siku uongozi hautakuwa kwenye mikono yake, na ambacho kinaweza kumfaa ni kuishi ndani ya mioyo ya watu ili wamtetee na kumpigania baadaye.
Waswahili wanasema ukiuwa kwa upanga nawe utakufa kwa upanga na malipo ni hapahapa duniani,ilikuwa ni january 16, 1996, rais Strasser naye alipinduliwa na msaidizi wake, Brigedia Jenerali Julius Maada Bio,
Baada ya kupinduliwa,ilibidi bwana Strasser akimbilie nchini Uingereza, ambapo akiwa huko akajiunga na Chuo Kikuu cha Warwick, kilichopo mjini Coventry, akaanza kusomea masomo ya sheria,huku akijinasibu kutaka kuwa wakili na kuja kuwatetea waafrika alioshindwa kuwatetea akiwa madarakani kama rais,
Baada ya mwaka mmoja wa masomo, Strasser aliishiwa fedha na kumbidi kuacha chuo,na kuingia mtaani nchini uingereza,
Maisha ya Uingereza yakawa magumu kwake na kuamua kukimbilia nchini Gambia,ambapo inadaiwa nako kukawa pagumu, mwishowe akaamua kurudi nchini mwake alipozaliwa yaani Sierra Leone mjini Grafton, mashariki mwa mji mkuu wa nchi hiyo Freetown.
Kazi ya kwanza ambayo Strasser aliifanya ni kuanzisha chuo kidogo cha kufundisha kompyuta na teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama),ambapo napo laana ya na dhambi ya kuwanyanyasa raia wakati akiwa rais ikazidi kumwandama na hatimaye maisha ya kuendesha chuo chake yakamshinda pia na baada ya kila kitu kwenda kombo, Strasser alirudi nyumbani kwa mama yake mzazi na kuishi kwenye banda la uani,ambapo mpaka sasa, akiwa na umri wa miaka 49 bado anaishi hapo bila kazi na kunywa pombe za kienyeji mtaani huku akiishi kwa kuombaomba bila kujali kama alishawahi kuwa rais wa taifa kubwa na tajiri kama Sierra Leone.
Naamini kila mmoja wetu aliesoma andiko hili atapata cha kujifunza.

No comments