Ads

Misaada yaanza kutolewa tena Misri, baada ya kusitishwa...............

Madhara ya vita Syria

Image copyright
Umoja wa Mataifa umefanikiwa kufikisha misaada ya kibinadamu katika kitongoji kinachokaliwa na waasi cha Moadamiya, Damascus.
Chakula na misaada mingine ya dharura kwa takriban watu elfu 40, ilipakuliwa ikiwa ni ya kwanza nchini humo tangu huduma hizo kusimamishwa kutolewa, kufuatia shambulio la mauaji lililofanywa karibu na mji wa Aleppo.
Mratibu wa Masuala ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa nchini Syria Jan Egeland amesema serikali ya Syria kwa sasa inaandaa vibali zaidi.
Amemtaka Rais wa Syria Bashar al- Assad kuruhusu msafara mwingine wa malori arobaini ambayo inasubiri kuelekea Aleppo kutokea katika mpaka wa Uturuki, na kusema kuwa chakula hicho kinaisha muda wa matumizi yake siku ya Jumatatu.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.