Ads

Marekani yaishutumu Urusi kuvunja mazungumzo ya amani Syria

Marekani na Urusi zinalaumiana kwa kuvunjika makubaliano ya amani

Balozi wa Marekani katika umoja wa mataifa, Samantha Power ameituhumu Urusi kwa kuzungumza uongo uliodhahiri kuhusu hatua yake nchini Syria.
Amesema kuwa Warusi hawakushirikishwa katika kupamana na ugaidi nchi Syria.
Vitaly Churk
Bi Power aliliambia baraza la usalama la umoja wa mataifa kwamba Urusi na Syria wanatekeleza vitendo vyote vya kimabavu dhidi ya upinzani uliopo Mashariki mwa Alepo, ndipo hapo uhalifu wa kivita unaweza kutekelezwa kwa kirahisi.
Kwa upande mwengine Balozi wa Urusi, Vitaly Churkin, amewatuhumu waasi kwa kuvunja makubaliano ya kusitisha vita ambayo yalishindikana ndani ya muda mchache tu.
Sehemu ya uharibifu uliotokana na vita

Mwakilishi wa Syria ameliambia baraza hilo la usalama kwamba jimbo lote la Alepo litarudishwa mikononi mwa serikali.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.