Ads

Ajib vs Mavugo sio watu wazuri Kabisa.......

Image result for simba sc

VS

Image result for mtibwa sugar






Magoli ya Ibrahim Ajibu na Laudit Mavugo yametosha kufanya Simba iendeleze ubabe mbele ya Mtibwa Sugar baada ya kuifunga kwa mara nyingine tena kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara.

Magoli yote ya Simba yamefungwa katika kipindi cha pili baada ya timu hizo kutoka sare katika dakika 45 za kipindi cha kwanza.

Mchezo huo uliwafanya Mzamiru Yassin nw Shiza Kichuya kucheza kwa mara ya kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar kwa mara ya kwanza tangu wasajliwe Simba msimu huu wa dirisha la usajili.

Ibrahim Mohamed ni mchezaji mwingine ambaye alisajiliwa Simba msimu huu akitokea Mtibwa lakini hakupata nafasi ya kucheza.


Katika mechi saba zilizopita, Mtibwa haijapata ushindi ushindi dhidi ya Simba. Imetoka sare kwenye mechi mbili na kupoteza mechi tano.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.