Maajabu ya paka huko Urusi
Paka amlea mwanatumbili Urusi
24 Agosti 2016
Mwanatumbili mmoja wa jamii ya tumbili wanaofanana na kuchakulo, ambaye alikataliwa na mamake, amekuwa akitunzwa na paka katika hifadhi moja ya wanyama Urusi.
Mkurugenzi wa hifadhi ya wanyama ya Tyumen ndiye aliyetoa wazo la wanyama hao kuishi pamoja.
Mwanatumbili huyo, aliyepewa jina Fyodor, alipowekwa na paka huyo kwa jina Rosinka ambaye ana miaka 16, waliibuka kuwa marafiki wakuu.
No comments