Ads

Mgao wa Fedha za Mbwana Samatta Kuuzwa Genk Zaanza Kuleta Zengwe Klabu ya Simba...


TP Mazembe imemuuza Mbwana Samatta kwa KRC Genk ya Ubelgiji ikadaka fedha zake, jambo la kushangaza hadi leo Simba haijalipwa sehemu ya fedha hizo kwa mujibu wa mkataba.
Simba ilipomuuza Samatta kwa TP Mazembe ya DR Congo, moja ya masharti ya mkataba ni kulipwa asilimia 20 ya kila anapouzwa lakini hadi sasa klabu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi haijapokea fedha za Genk.

Ili kujiridhisha kabla ya kuchukua hatua zaidi, Simba ilifanya uchunguzi ikiwemo kuwasiliana na Genk na kuhakikishiwa kuwa, tayari waliilipa TP Mazembe fedha zote za usajili.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.