Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 26.01.2018
Mshambuliaji wa Paris St-Germain na Brazil Neymar ataruhusiwa kujiunga na Real Madrid, lakini kwa makubaliano ya iwapo ataisaidia timu hiyo ya Ufaransa kubeba kombe la vilabu bingwa Ulaya kulingana na rais wa timu hiyo Nasser Al-Khelaifi .Mchezaji huyo mwenuye umri wa miaka 25 ana ndoto ya kuichzea timu hiyo. (Goal)
Mazungumzo yamegonga mwamba kati ya Arsenal na Borussia Dortmund kuhusu makubaliano ya mshambuliaji wa klabu hiyo na Garbon Pierre -Emrick Aubameyang kwenda Arsenal.
Dortmund pia inatarajiwa kusitisha majadiliano ya kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud .Mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 31 anadaiwa kutaka kushirikishwa katika kila mechi. (Mail)
Chelsea inataka kumsajili Giroud , ikiwa na matumani ya kutaka kumshawishi kuhamia magharibi mwa mji huo. (Mirror)
Manchester City inatarajia kukamilisha usajili wa beki wa Athletic Bilbao Aymeric Laporte wikendi hii. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 amebadilisha nia yake baada ya kukataa uhamisho wa kueleka City miezi 18 iliopita.{Mirror}
Wakati huohuo mmiliki wa Chelsea Abrahamovic amekasirishwa na mkufunzi Conte baada ya kocha huyo kujitenga na usajili wa mchezaji mpya msimu huu. (Star)
Winga wa PSG Brazil Lucas Moura, 25, alikutana na mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy mjini London siku ya Alhamisi kuzungumzia uhamisho wa kuelekea Spurs. (RMC - in French)
Diafra Sakho ameiambia West Ham anataka kuondoka na klabu ya Ufaransa ya Rennes ndio anakoelekea . Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kutoka Senegal hajashirikishwa katika mechi nyingi za West Ham msimu huu (Sun)
West Ham inalenga usajili wa nahodha wa Fulham Tom Cairney na wako tayari kutoa dau la £15m kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kutoka Uskochi. (Sky Sports)
West Ham imewasilisha ombi la £12m kumsajili kiungo wa kati wa Norwich na Uingereza James Maddison, 21. (Guardian)
HUU NDIO MWISHO WA URAFIKI WA DIAMOND NA RICHROUSE
Ombi la pili la Crystal Palace kutaka kumsajili beki wa Lille Ibrahim Amadou limekataliwa. Palace ilikuwa imehusishwa na uhamisho wa mchezaji huyo wa Cameroon mwenye umri wa miaka 24 mapema mwaka huu. (Sky Sports)
Mshambuliaji wa zamani wa Fulham, Reading na Urusi Pavel Pogrebnyak, 34, alichiliwa na Dynamo Moscow kwa sababu ya kuhudhuria mechi ya Juventus nchini Itali , licha kuambia klabu hiyo kwamba alikuwa mgonjwa sana kuichezea (Sport Express - in Russian)
Mshambuliaji wa Leicester na Uingereza Jamie Vardy anatarajiwa kukabiliana na ,mwanafunzi aliyehitimu kutoka chuo chake cha soka cha V9 Academy, Alex Penny, wakati Leicester itakapocheza dhidi ya Peterborough katika kombe la FA raundi ya nne siku ya Jumamosi. (Sky Sports)
Mkufunzi wa Tottenham Mauricio Pochettino anasema kuwa angependelea kufanyakazi katika shamba badala ya kuifunza Arsenal au Barcelona , lakini raia huyo wa Argentina ambaye ana umri wa miaka 45 hajapinga kuelekea Real Madrid.(Express)
Arsenal wanajiandaa kumsajili kiungo wa kati wa Corinthians na mchezaji wa timu ya Brazil isiozidi umri wa miaka 20 Maycon, 20. (Sun)
Mkufunzi wa Leicester Claude Puel anasema kuwa winga Riyad Mahrez hatahamia klabu nyengine yoyote wakati wa dirisha la uhamisho la mwezi Januari. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kutoka Algeria alipigwa picha akiwa katika uwanja wa Emirates akitazama mechi ya kombe la Carabao kati ya Arsenal na Chelsea siku ya Jumatano, lakini Puel amesisitiza kuwa anawatafutia wachezaji Leicester. (Mirror)
Sandro Ramirez ameambia Everton anataka kuondoka katika klabu hiyo. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kutoka Uhispania yuko tayari kurudi nyumbani huku klabu ya La Liga ya Sevilla ikimnyatia. (Mail)
Kiungo wa kati wa West Brom na Ireland Kaskazini Chris Brunt, 33, anakaribia kusaini kandarasi mpya katika klabu hiyo.(Birmingham Mail)
No comments