Kenyatta ateua mawaziri wapya Kenya.....
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza watu anaopendekeza waidhinishwe kuwa mawaziri katika serikali yake mpya baada yake kushinda uchaguzi mwaka jana.
Mawaziri sita ambao walikuwa wanahudumu katika serikali yake muhula uliopita wamevuliwa uwaziri na kuteuliwa kuwa mabalozi.
Bw Dan Kazungu, ambaye amekuwa waziri wa madini, amependekezwa kuwa balozi mpya wa Kenya nchini Tanzania.
Aliyekuwa balozi wa Kenya nchini humo Chirau Ali Mwakwere alijiuzulu mwaka jana ili kuwania kiti cha ugavana katika uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti.
Alishindwa kwenye uchaguzi huo.
Miongoni mwa walioteuliwa kuwa mawaziri wapya ni mwanahabari mkongwe Farida Karoney ambaye ameteuliwa kuwa waziri wa ardhi.
Wadhifa huo ulikuwa unashikiliwa na Prof Jacob Kaimenyi ambaye amependekezwa kuwa balozi wa Kenya katika Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Sayansi, Elimu na Utamaduni (Unesco) mjini Geneva.
Bi Monica Juma ameteuliwa kuwa waziri mpya wa mambo ya nje kuchukua nafasi ya Amina Mohamed ambaye amependekezwa kuwa waziri wa elimu.
Mawaziri walioteuliwa kuwa mabalozi
- Judi Wakhungu (Mazingira) - Ufaransa
- Cleopa Mailu (Afya) - Umoja wa Mataifa mjini Geneva
- Dan Kazungu (Madini) - Tanzania
- Phylis Kandie (Leba na Jumuiya ya Afrika Mashariki) - Ubelgiji, Luxemburg na Umoja wa Ulaya
- Willy Bett (Kilimo) - India
- Jacob Kaimenyi (Ardhi) -UNESCO, Paris
- Hassan Wario (Michezo) - Austria
Kwa sasa, orodha kamili ya mawaziri waliopendekezwa ni:
- Adan Mohammed - Viwanda
- Amina Mohammed - Elimu
- Charles Keter - Kawi
- Eugene Wamalwa - Ugatuzi
- Farida Karoney - Ardhi
- Fred Matiangi - Masuala ya Ndani na Usalama
- Henry Rotich - Fedha (Hazina Kuu)
- James Macharia - Uchukuzi
- John Munyes - Madini na Mafuta
- Joseph Mucheru - Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
- Keriako Tobiko - Mazingira
- Margaret Kobia - Vijana na Utumishi wa Umma
- Monica Juma -Mambo ya Nje
- Mwangi Kiunjuri - Kilimo
- Najib Balala - Utalii
- Peter Munya - Jumuiya ya Afrika Mashariki
- Racheal Omamo - Ulinzi
- Raphel Tuju - Waziri (Bila wizara kwa sasa)
- Rashid Achesa - Michezo
- Sicily Kariuki - Afya
- Simon Chergui - Maji
- Ukur Yattany - Leba
No comments