Yaliyojiri Leo Huko Ulaya kwenye MIchezo na mwandishi wako ally mshana
Manchester United wanahamu kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Watford mwenye umri wa miaka 25, Abdoulaye Doucoure lakini wanakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka kwa Liverpool, Tottenham na Arsenal. (Mirror)
Mshambuliaji wa zamani wa Uholanzi Patrick Kluivert anajadiliana na Oxford United kuhusu kuwa meneja mpya wa klabu hiyo. (Sun)
Liverpool inakaribia kufikia makubaliano na Monaco ya winga Thomas Lemar mwenye umri wa miaka 22. (Le 10 Sport, via Metro)
Manchester United ndio wanaopigiwa upatu kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Juventus Blaise Matuidi, katika msimu huu wa joto. (Star)
Watford, Liverpool, Arsenal na West Ham wote wanamwinda mchezaji wa kiungo cha kati wa Benfica Bryan Cristante. Hatahivyo , raia huyo wa Italia anatarajiwa kwanza kukamilisha uhamisho kwenda Atalanta, ambako kwa sasa yuko kwa mkopo. (Tuttosport, via Watford Observer)
Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Argentina Pablo Dybala, mwenye umri wa miaka 24, anayelengwa na Manchester United, Barcelona na Real Madrid, atasaini mkataba mpya wa miaka mitano na Juventus usiojumuisha kipengee cha lini atakapoachiwa. (Sun)
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola ametilia uzito kumtafuta mrithi wa mchezaji wa kiungo cha kati raia wa Brazil Fernandinho, mwenye umri wa miaka 32, katika msimu ujao wa joto. (Manchester Evening News)
Muungano wa mashabiki wa Arsenal - wanatarajiwa kukutana na afisa mkuu mtendaji wa klabu hiyo Ivan Gazidis mwishoni mwa juma hili kuwasilisha matokeo ya utafiti uliobaini kuwa 88% ya mashabiki waliopiga kura wanataka wakuu wa klabu hiyo wamtimue meneja Arsene Wenger msimu huu wa joto. (London Evening Standard)
Aliyekuwa mchezaji wa kiungo cha kati wa Arsenal Ray Parlour anasema mmiliki wa Gunners Stan Kroenke hana wasiwasi na matolkeo ya klabu hiyo, na badala yake lengo lake ni kupata pesa. (Talksport)
Wakati huo huo, meneja wa Arsenal Arsene Wenger hayupo tena katika orodha ya watu wanaowindwa na Paris St-Germain, kwa mujibu wa mwandishiw a michezo wa Ufaransa Julien Laurens. (5 live Football Daily)
Beki wa Chelsea Marcos Alonso anasema aliyekuwa mkuu wa Barcelona Luis Enrique "ni bora kwa kalbu yoyote", wakati Mhispania huyo akipigiwa upatu kumrithi meneja wa the Blues Antonio Conte. (Cope, via Mirror)
Mchezaji wa kiungo cha kati wa timu ya Schalke Max Meyer huenda akajiunga na Atletico Madrid katika uhamisho wa bure msimu huu wa joto. Mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 raia wa Ujerumani unamalizika Juni. (Bild, via Mail)
Beki wa Bayern Munich David Alaba, anaweza kufanyiwa uhamisho kwenda Barcelona, huku raia huyo wa Austria akisema anawaza kutafuta changamoto mpya". (Kurier, via IBT)
Juventus hawako tayari kumuuza mchezaji Winger Juan Cuadrado kwa bei yoyote. (Calciomercato)
No comments