Zaidi ya 300 wajeruhiwa wakati wa kura ya uhuru Catalonia
Maafisa huko Catalalonia wanasema kuwa watu 337 wamejeruhiwa kwenye ghasia wakati polisi wanajaribu kuzuia kura ya maoni ya uhuru wa Cataloniahttps://youtu.be/9VSTC_-KzzI
Serikali ya Uhispania imeahidi kuzuia kura hiyo ambayo imetangazwa kuwa isiyo halali na mahakama ya katiba ya nchi hiyo.
Maafisa wa polisi wanawazuia watu kupiga kura huku wakichukua makaratasi ya kupigia kura na masanduku kutoka kwa vituo vya kupigia kura.
Maafisa wa serikali ya Catalonia wametabiri idadi kubwa ya watu kujitokeza.
Makatasi ya kipigia kura yana swali moja tu: "Unataka Catalonia kuwa taifa huru na jamhuri?" Kuna masanduku mawili ya ndio na hapana.
Katika mji wa Girona polisi wa kuzima ghasia waliingi katika vituo vya kupigia kura kwa nguvu ambapo kiongozi wa eneo hilo alitarajiwa kupigia kura yake.
Picha za televisheni ziliwaonyesha wakivunja vioo vya kuingia kituo hicho na kuwaondoa kwa nguvu wale waliojaribu kupiga kura.
Hata hivyo shirika la habari la Reuters lilisema kuwa Bw Puigdemont alifanikiwa kupiga kura yake.
Wakati huo huo kwenye mji mkuu wa eneo hilo, Barcelona polisi walifyatua risasi za mipira kwa wale wanaounga mkono hatua ya kujitenga.
No comments