Tetesi za soka Ulaya Jumatano 04.10.2017
West Ham na Everton wanamtaka mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcot ,28, ambaye huenda asiongeze kandarasi yake Arsenal iwapo ataendelea kukalia benchi.(Sun)
Manchester City wanakabiliwa na upinzani mkali wa kumzuia kocha Patrick Viera huku raia huyo wa Ufaransa akidaiwa kuvutiwa na klabu ya Saint-Etienne(Manchester Evening News)
Real Madrid wanaandaa kitita cha Yuro milioni 200 kumsajili mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane.
Mabingwa hao wa Ulaya na Uhispania hawajazuiwa na ombi la kitita cha juu kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 .(Don Balon - kwa Uhispania)
Manchester United wanatumaini la kumsajili kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil ,28, wakati kandarasi yake itakapokamilika mwisho wa msimu huu. (Independent)
Meneja Antonio Conte huenda akaihama Chelsea na kuelekea AC Milan mwishowe wa msimu huu.
Mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 48 ameiambia idhaa moja ya Itali kwamba anatamani kurudi nyumbani. (Sun via Corriere dello Sport)
Hatahivyo, The Blues wako tayari kumununua beki wa kushoto wa Juventus Alex Sandro ,26, ili kumzuia kocha huyo kuondoka katika klabu hiyo. (Mirror)
Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero huenda akakosa wiki mbili zaidi baada ya kupata jeraha la mbavu.
City ilikuwa na matumaini kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 atashiriki mechi ya kwanza baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa. (Daily Mail)
Arsenal inamsaka Kepa Arrizabalaga ambaye anaelekea kutia saini kandarasi mpya Atletico Bilbao.
Kipa huyo mwenye umri wa miaka 23 alihusishwa na uhamisho wa Arsenal na Real Madrid (Talksport via Marca)
Manchester United na Chelsea wanamsaka beki wa Middlesbrough Dael Fry, 20. (TeamTalk)
Klabu ya ligi ya daraja la kwanza Leeds inamsaka mshambuliaji wa Liverpool ,25, Danny Ings (ESPN)
Aliyekuwa mkufunzi wa Manchester United Louis van Gaal amehusishwa na uhamisho wa Bayern Munich, baada ya Carlo Ancelotti kufutwa kazi wiki iliopita. (mirror)
Mshambuliaji wa wa Manchester City Leroy Sane, 21, aliweka rekodi ya kukimbia kwa kasi zaidi tangu ligi ya Uingereza kuanzishwa. (Manchester Evening News)
Paul Pogba, 24, amepigwa marufuku kutoshiriki mpira wa vikapu na Manchester United ili kuzuia kupata majeraha zaidi.. (Sun)
Urusi imetengeza eneo la kukalia nje ya uwanja mmoja utakaotumika katika kombe la dunia, the Ekaterinburg Arena, ili kuafikia masharti ya Fifa (Yahoo Sports)
Mchezaji wa zamani wa Tennis Andy Murray atajaribu kuwa mkufunzi wa soka iwapo hatoendelea kucheza tenisi. (Goal.com kupitia Fifa.com)
Naibu mkufunzi wa Jamhuri ya Ireland Roy Keane amewaonya wachezaji wanaoogopa majeraha ya kichwa kucheza mchezo wa Chess badala yake. (Telegraph)
Tajiri Amanda Staveley amekutana na maafisa wa klabu ya Newcastle na ameanzisha mawasiliano kwa mazungumzo zaidi kuhusu kuinunua klabu hiyo (The Daily Telegraph)
Barabara moja mjini Setubal Ureno imetajwa jina la mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho (Daily Mail)
Mkufunzi huyo wa Man United hataki mshambuliaji Marcus Rashford kutumiwa katika mechi mbili za kufuzu kwa kombe la dunia wiki hii.(Daily Express)
Stan Kroenke, ambaye ana hisa nyingi katika Arsenal amewasilisha ombi la kununua hisa za mwanahisa wa pili kwa ukubwa katika klabu hiyo Alisha Usmanov kwa £525m (Guardian)
Wachezaji wa Arsenal waliwachwa wakiwa na hasira baada ya kiungo wa kati Mesut Ozil na mshambuliaji Alexis Sanchez kulifeli kushiriki katika mkutano wa klabu hiyo na wanahabari mwezi uliopita.. (Evening Standard)
Mchezaji wa Hull City' Ryan Mason amemshkuru kipa wa Arsenal Petr Cech kwa kumsaidia baada ya Mason kupata jeraha la kichwa Januari iliopita. (Sun via Talksport)
Mshambuliaji wa Chelsea Michy Batshuayi aliimbiwa na wachezaji wenzake alipokuwa akisherehekea siku yake ya 24 ya kuzaliwa . (Daily Mail)
No comments