Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 05.10.2017
Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane, 24, anasema kuna uwezekano wa yeye kuhamia Real Madrid (Express)
Spurs itashindana na Chelsea katika kumsajili kiungo wa kati wa Everton Ross Barkley (Mirror)
Bayern Munich itamwajiri kocha Jupp Heynckes, 72, ambaye aliiongoza timu hiyo kushinda matatji matatu 2013 kama mkufunzi mpya. (Bild - in German)
Manchester City huenda ikaipiku Manchester United kumsajili kiungo wa kati wa New York City Jack Harrison.
Kikosi hicho cha Pep Guardiola's kiko kifua mbele kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 kutokana na ushirikiano wao na klabu ya MLS nchini Markni. (Sun)
Mshambualiji wa Fenerbahce's, 34, Robin van Persie atarudi Feyenoord, klabu ya Uholanzi ambayo alianza kuichezea. (Aksam- in Turkish)
Mshambuliaji wa Chelsea Michy Batshuayi, 24, huenda akafaulu pakubwa baada ya Eden Hazard kumshauri kusalia katika klabu hiyo katika msimu ujao. (DH.BE, via ESPN)
Washambuliaji Ben Woodburn, 17, na Roberto Firmino, 26, wanatarajiwa kuweka kandarasi mpya za muda mrefu na Liverpool. (Liverpool Echo)
Manchester United wanakaribia kukubaliana na kiungo wa kati Marouane Fellaini, 29 kuingia katika mkataba mpya. (Transfermarketweb)
Chelsea na Liverpool wanamsaka kiungio wa kati wa Paris St-Germain Javier Pastore. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28-year- ameambiwa anaweza kuondoka mwezi Januari. (El Gol, via Talksport)
Crystal Palace na Fulham zinamnyapia kinda Lex Allan,18, anayechezea klabu ya Sittingbourne katika ligi ya Bostik na amekuwa akifanya mazoezi na timu ya daraja la kwanza Millwall. (Kent Online)
Inter Milan inalenga kumsajili winga wa Arsenal Theo Walcott mnamo mwezi Januari. Mchezaji huyo mweny umri wa 28- amekuwa na Arsenal tangu mwaka 2006 (Calciomercato, via Talksport)
Gareth Southgate atapokea marupurupu zaidi ya £250,000 iwapo Uingereza itafuzu katika kombe la dunia kwa kuishinda Slovenia katika uwanja wa Wembley siku ya Alhamisi. (The Times - subscription required)
Mshambuliaji wa Everton Wayne Rooney, 31, ambaye amestaafu katika soka ya kimataifa amepokea barua ilioandikwa na mwenyekiti wa shirikisho la soka nchini humo FA Greg Clarke akimshukuru kwa huduma yake katika timu ya Uingereza.(Daily Star)
Beki wa Uingereza Michael Keane, 24, aliharibu vifaa vya kamera vilivyo na thamani ya £10,000 wakati ambapo mpira aliokuwa akitumia wakati wa mazoezi kugonga uzio.(Daily Mail)
Beki wa Manchester United Victor Lindelof anasema kuwa amefanya mazungumzo na mkufunzi Jose Mourinho, licha ya kutoanzishwa katika mechi ya ligi ya Uingereza.. (Expressen - in Swedish)
Facebook imesema kuwa kuna uwezekano ikawasilisha ombi la kutaka haki za kuonyesha mechi za ligi ya Uingereza. (Guardian)
Kipa wa Tottenham Hugo Lloris amemuonya kwa utani mchezaji mwenza wa Ufaransa na mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud kwamba ''kuna mshambuliaji mpya mjini''.. (Instagram)
Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola anamtambua atakayekuwa kocha mpya wa klabu ya Bayern Munich, amesema rais wa klabu hiyo.(Sky Sports)
Uwanja wa kombe la dunia la 2018 huko Ekaterinburg, Urusi, utakuwa na viti vya muda nje ili kuafikia masharti ya idadi ya viti ya Fifa. (Guardian)
Mmiliki wa asilimia 30 ya hisa za Arsenal Alisher Usmanov anasema kuwa hatomuuzia hisa hizo mmiliki mkubwa wa klabu hiyo Stan Kroenke lakini anaweza kufanya hivyo kwa mtu mwenye maono sawa na yake kuhusu klabu hiyo. (Telegraph)
Mkufunzi wa Ubelgiji Roberto Martinez anasema kuwa hatohatarisha hali ya mechezaji wa Manchester United Romelu Lukaku. (Telegraph)
SIKIA ALICHOKISEMA AKILI MALI JUU YA WALE WANAOMSEMASEMA
No comments