Ads

MWENYEKITI NA WAJUMBE KAMATI TFF BADO TAFRANI...



Image result for jamali malinzi
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi wa TFF, Revocatus Kuuli amesema
yuko tayari kujiuzuru baada ya kutofautiana na wajumbe wake juu ya hatma ya rais anayemaliza muda wake Jamal Malinzi.
Kamati ya Uchaguzi ya TFF ina wajumbe watano kati ya hao watatu na Makamu mwenyekiti Domina Madeli  wanataka Malinzi apitishwe bila ya kuwepo jambo linalopigwa na  mwenyekiti Kuuli.
Katika usahili huo wagombea 70 wamepitishwa kati ya 72, lakini ilipofika wakati wa kujadili jina la Malinzi ndipo wajumbe walipotofautina.
Akizungumza baada ya kuvunja kikao hicho Kuuli alisema usahili ulienda vizuri kwa wagombea wote, uamuzi wa kutumika busara kwa rais Malinzi umesababisha kutoelewana kwa wajumbe na kusababisha amvunja kikao hicho hadi kesho, Jumapili.
Kuuli alisema baadhi ya wajumbe wametaka busara itumike kwa wagombea ambao hawapo yaani Malinzi kuwa apitishwe hata kama hayupo na vielelezo vyake viletwe na mtu mwingine.
Kuuli alisema anaheshimu mawazo ya wenzake ila  dhamira yake inamtuma kusimamia ukweli.
"Mtu hawezi kupitishwa wakati hakuwepo katika usahili na huo ndiyo msimamo wangu na kesho
Jumapili litaendelea kujadiliwa katika kikao hiki.
"Tukishindwana basi mimi nitajiuzuru kuwa  mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa TFF kwa sababu nina kazi nyingine za kufanya," alisema Kuuli.
WAPITISHWA KUWANIA NAFASI MBALIMBALI TWFA

Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu kwa Wanawake (TWFA), imetangaza majina ya wagombea 11 waliopitishwa kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu wa chama hicho utakaofanyika Agosti 5, mwaka huu mkoani Morogoro.

Majina ambayo yamepitishwa ni Amina Karuma, Rose Kisiwa, Somoe Ng’itu, Theresia Mung’ong’o, Hilda Masanche, Salma Wajeso, Zena Chande, Triphonia Temba, Mwamvita Kiyogoma, Jasmin Soudy na Chichi Mwidege.

Nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.