KOREA KASKAZINI YARUSHA KOMBORA JAPAN...
Korea Kaskazini imerusha kombora jingine la masafa marefu kutoka jimbo lake la magharibi kulingana na mamlaka ya Japan na Korea Kusini.
Kombora hilo lilirushwa kutoka Bangyon Kaskazini mwa mkoa wa Pyongan kulingana na chombo cha habari cha Yonhap kikitaja duru za jeshi la Korea kusini.
Tokyo imesema kuwa kombora hilo huenda lilianguka katika eneo la kiuchumi la bahari ya Japan.
Korea Kaskazini imeongeza viwango vya majaribio vya makombora yake katika meizi ya hivi karibuni hatua inayoendelea kuzua wasiwasi.
Kombora hilo la siku ya Jumanne lilisafiri umbali wa kilomita 930 kwa dakika 40,kulingana na Korea Kusini na Japan.
- Abe aishutumu Korea Kaskazini kwa kurusha kombora
- Kombora jingine la Korea Kaskazini lafeli majaribio
- Uwezo wa kombora jipya la Korea Kaskazini
Hili ni kombora la 11 lililogunduliwa mwaka huu lakini urefu wake umeongezeka kulingana na mwandishi wa BBC mjini Seoul Stephens Evans.
Mara ya mwisho Korea Kaskazini ilifanyia majaribio kombora lake mnamo mwezi Mei.
Ilirusha makombora yake katika wakati tofauti, yote yakielekezwa bahari ya Japan.
Waziri anayesimamia maswala ya serikali nchini humo Yoshihide Suga aliambia maripota:Uchokozi kama huu wa Korea kaskazini hauwezi kukubalika.Tuliwasilisha malalamishi yetu na kushutumu hatua hiyo.
Rais mpya wa Korea Kusini aliyechaguliwa hivi majuzi ametaka kufanywa kwa mkutano wa dharura katika baraza la usalama la taifa hilo.
- Korea Kaskazini yaonywa kuthubutu kurusha makombora
- Marekani kufanya majaribio ya kudungua kombora
- Korea Kaskazini yashutumiwa kwa kulipua bomu
Bwana Moon pia alikutana na rais Trump wiki iliopita, huku kiongozi huyo wa Marekani akiionya Pyongyang kwamba itapata jibu sahihi.
Kurushwa kwa kombora hilo kunajiri siku moja baada rais Donald Trump kuzungumza katika simu na waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe na rais wa China Xi Jinping kuhusu Korea Kaskazini.
Viongozi hao walithibitisha jitihada zao za kuhakikisha kuwa hakuna utumizi wa nyuklia katika rais ya Korea
No comments