MAAJABU SABA YA JEZI NUMBER SABA UWANJANI..

1. CRISTIANO RONALDO
FC Bayern Muenchen v Real Madrid - UEFA Champions League
Semi Final
Star wa Real Madrid anafunga list hii ya wachezaji waliowahi
kupata mafanikio wakiwa ndani ya jezi namba 7 huku akiwa bado na muda wa
kuendelea kufanya makubwa zaidi.
Akianza kupata mafanikio kwenye klabu ya Manchester United,
mreno huyo mwenye kipaji cha aina yake alihamia Hispania mwaka 2009 na
ameendelea rekodi ya kufunga magoli ambayo itawachukua muda mrefu ma-striker
kuivunja.
Lakini Ronaldo bado hajashinda taji lolote akiwa mchezaji wa
timu ya taifa ya Ureno, mambo yote hayo makubwa ambayo Ronaldo ameyafanya
kwenye soka akiwa amevaa jezi namba 7.
2. GARRINCHA
Garrincha
Garrincha ni jina maarufu kwenye soka la Brazil, anasimama
kama mchezaji bora kuwahi kutokea amabaye alikuwa akivaa jezi namba 7. Akiwa
amekiongoza kikosi cha Seleccao kutwaa kombe la dunia mwaka 1972 bila ya Pele.
Garrincha alikuwa pia nyota wa klabu ya Botafogo.
Legend huyo wa Brazil alichaguliwa kwenye timu ya karne ya
20 na timu ya FIFA ya muda wote ya kombe la dunia.
3. CANTONA
Cantona
Akiwa anatambulika kwa a.k.a ya ‘Premier League bad boy’,
Eric Cantona ni miongoni mwa majina yenye heshima kuwahi kuvaa jezi namba 7 ya
United.
Licha ya kuchukiwa na baadhi ya mashabiki, Cantona
alifanikiwa kuwateka mashabiki wengi wa United kutokana na kiwa alichokuwa
anakionesha uwanjani. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa alidumu United kwa
miaka 5 lakini aliweza kufunga magoli 80 na kushinda mataji kibao ikiwemo ya
mataji matatu (treble) ya mwaka 1999.
4.KENNY DANGLISH
Dalgrish

Kenny Danglish alikuwa ni miongoni mwa wachezaji muhimu
ndani ya Liverpool kwenye miaka ya 1970 na 80 na anatambuliwa kama miongoni ya
wachezaji bora kuwahi kuitumikia Liverpool.
Alichukua namba 7 ambayo ilikuwa inavaliwa na mkongwe mwingi
wa Liverpool Kevin Keegan, lakini alifanikiwa kupata mafanikio kuliko
alyemtangulia kuvaa jezi hiyo.
5. GEORGE BEST
Best

George Best ni nyota mwingine wa Manchester United,
alithibitisha jina lake kwa uwezo wake uwanjani katika miaka yote aliyocheza
soka.
Mu-Ireland huyo alikuwa na uwezo wa kucheza nafasi ya kiungo
wa kati na winger, alikuwa kwenye kiwango bora kati ya 1966-72 ambapo
aliiongoza United kutwaa mataji ndani na nje ya England huku akifanikiwa
kushinda tuzo binafsi.
6. LUIS FIGO
Figo
Nahodha wa aina yake kuwahi kutokea kwenye timu ya taifa ya
Ureno ambaye alikuwa akivaa jezi namba 7 na kupata mafanikio makubwa. Winga
mwenye uwezo wa juu kipindi cha uchezaji wake, anasifika kwa uwezo wake mkubwa
wa kukimbia na mpira huku akiwaacha mabeki huku akiwa na uwezo mkubwa wa
kutengeneza nafasi kwa wachezaji wenzake kufunga.
Nyota huyo wa Ureno atakumbukwa wakati anakitumikia kikosi
cha Inetr Milan na Real Madrid licha ya kushindwa kutwaa taji lolote akiwa na
timu yake ya taifa lakini anabakia kuwa miongoni wachezaji bora kuwahi kutokea
Ureno.
7. PIRES
Pirez
Robert Pires alidumu kwenye kikosi cha Arsenal kwa miaka 6
pekee lakini ilitosha heshima kwenye klabu hiyo na kuwa miongoni mwa wachezaji wa
kukumbukwa kwenye historia ya Arenal.
Baada ya mafanikio makubwa kwenye michuano ya kombe la dunia
na Euro mwaka 1998 na 2000 akiwa na timu ya taifa ya Ufaransa, Pires alijiunga
na The Gunners na kukiongoza kikosi hicho kutwaa kombe makombe matatu ya FA na
mataji mawili ya Premier League.
Kutokana na mchango wake kwenye kikosi cha Arsenal katika
miaka 6 aliyoitumikia, alichaguliwa na mashabiki kama mchezaji wa sita mwenye
mchango mkubwa kwenye timu.
No comments