Ads

Kipa Mbao FC aeleza sababu za kudondoka Uwanjani vs Yanga SC....

Benedict Haule ni moja ya majina yaliyokuwa gumzo sana Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2016/17 akiwa kipa wa Mbao FC lakini lipo kubwa ambalo lilikuwa gumzo zaidi baada ya kudondoka uwanjani kwenye mchezo dhidi ya Yanga SC uliopigwa CCM Kirumba, Mwanza ambapo walishinda bao 1-0.
Ayo TV na millardayo.com zimemtafuta Benedict Haule ambaye anafunguka zaidi kuhusu tukio hilo kwenye VIDEO hii ambayo unaweza kuitazama kwa kubonyeza PLAY…
“…hapana ile ilitokea baada ya Busou mchezaji wa Yanga alinipiga ndiyo maana nikapata maumivu nikadondoka chini lakini pale golini hapana kitu chochote. Zaidi sisi tulikuwa tunacheza na mind yao kwamba kuna kitu ili wenyewe waweze kupanic ili sisi tuweze ku-win mchezo.” – Benedict Haule.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.