Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 17.01.2018
Chelsea wamezungumza na West Ham kuhusu kumsaini mshambuliaji wa miaka 29 Andy Carroll kwa mkataba wa kudumu. (Telegraph)
West Ham wanataka kuskiliza ofa ya pauni milioni 20 kwa Carroll. (Sky Sports)
Kiungo wa kati raia wa Armenia, Henrikh Mkhitaryan, 28, anasema anataka nyongeza ya mshahara kuweza kuhama Manchester United kwenda Arsenal. (Mirror)
Everton wanatarajiwa kumaliza kumsajili wing'a wa Arsenal na England Theo Walcott, 28, leo Jumatano. (Liverpool Echo)
Mshambujia raia wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 28, anaiomba Borussia Dortmund kumruhusu ajiunge na Arsenal. (Mirror)
Kiungo wa kati wa Arsenal na England Jack Wilshere, 26, ambaye mkataba wake unakamilika msimu huu ni lazima afanyiwe uchunguzi wa kiafya na kukubali mshahara wake kupunguzwa kwa asilimia 20 kuweza kupata mkataba mpya. (Sun)
Barcelona wamekataa ofa ya pauni milioni 22.2 kutoka Inter Milan kwa raia wa Brazil mwenye umri wa miaka 24 Rafinha kwa sababu wanataka pauni milioni 35.5.
Cardiff wamefanya mazungumzo na Bournemouth kuhusu kusainiwa kwa mshambuliaji Lewis Grabban, 30. (Bournemouth Echo)
Mshambuliaji wa Manchester United Henrikh Mkhitaryan, 28, yuko huru kuhama kwenda London kujiunga na Arsenal. (Mirror)
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger ana wasi wasi kuhusu kumsaini mshambuliaji mwenye hasira wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang. (Star)
Tottenham ni kati ya vilabu vinavyommzea mate mchezaji wa hadhi juu wa Norwich James Maddison, 21. (London Evening Standard)
Kiungo wa kati wa Liverpool raia wa Serbia Marko Grujic, 21, analengwa kwa mkopo na Middlesbrough na Cardiff City. (ESPN)
Mshambuliaji wa Southampton Manolo Gabbiadini, 26, anataka kurejea kwa moja ya vilabu vyake vya zamani Bologna. (Sky Italia, via Talksport)
Tottenham ni kati ya vilabu vinavyomtaka kiungo wa kati wa Norwich City James Maddison. (Evening Standard)
Fulham wako kwenye mazungumzo na mchezaji wa umri wa miaka 31 raia wa Argentina Sebastian Leto. (Daily Mail)
No comments