Ads

Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 11.01.2018

Winga wa Arsenal Theo WalcotHaki miliki yaEverton imejiunga na vilabu vilivyo na hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcot 28.
Muingereza huyo pia anasakwa na klabu yake ya zamani Southampton huku Arsenal ikidaiwa kutaka dau la £30m. (Liverpool Echo)
Mchezaji wa RB Leipzig na kiungo wa kati wa Guinea Naby Keita huenda akajiunga na Liverpool mwezi huu.Haki miliki ya picha
Mchezaji wa RB Leipzig na kiungo wa kati wa Guinea Naby Keita huenda akajiunga na Liverpool mwezi huu.
Liverpool tayari wamemsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kwa dau la £48m lakini wanaweza kulipa kati ya Yuro milioni 15-20 ili kumchukua kabisa.(Bild - in German)
Mkufunzi wa Jamhuri ya Ireland Kaskazini Martin O'Neill
Mkufunzi wa Jamhuri ya Ireland Kaskazini Martin O'Neill alitarajiwa kukutana na maafisa wa klabu ya Stoke siku ya Jumatano kuhusiana na wadhfa wa mkufunzi ulio wazi huku naibu wake Roy Keane pia akitarajiwa kuondoka iwapo atachukua wadhfa huo. (Irish Independent)
Guangzhou Evergrande wanasema kuwa hawatashindana na klabu pinzani ya ligi ya Super Beijing Guoan kupata hudumu za mchezaji wa Gabon na Borussia Dortmund Pierre Emerick Aubameyang (ESPN)
Dele Alli ni kiungo wa kati wa klabu ya Tottenham
Tottenham imeanza mazungumzo yasio rasmi na kiungo wa kati Dele Alli. Klabu hiyo inadaiwa kuwa na matumaini ya kutia saini kandarasi mpya na mchezaji huyo wa Uingereza. (Daily Mirror)
Naibu mwenyekiti wa klabu ya Fullham Tony Khan amesema kuwa beki wa kushoto wa klabu hiyo Ryan Sessegnon, 17, hatauzwa licha ya kusakwa na Manchester United na Tottenham Hotspurs. (Daily Telegraph)
Manchester United italazimika kulipa hadi £27m ili kumsajili kiungo wa kati wa Ubelgiji Leander Dendoncker kutoka Anderlecht mnamo mwezi Januari.(Manchester Evening News)
Mshambuliaji wa West ham na Senegal Diafra SakhoHaki miliki ya picha
Crystal Palace huenda ikakamilisha usajili wa mshambuliaji wa Senegal Diafra Sakho, 28, kutoka West Ham mwishoni mwa wiki . (Daily Mirror)
Huddersfield imekubali kuingia mkataba na winga wa Norwich Alex Pritchard, 24. Raia huyo wa Uingereza aliondoka Tottenham kwa dau la £8m katika dirisha la uhamisho la 2016. (Daily Mail)
West Ham wameambiwa watalazimika kulipa £15m ili kumsajili kiungo wa kati wa Bournemouth na Republic of Ireland Harry Arter, 28. (Daily Mirror)
Kiungo wa kati wa Real Madrid Dani Ceballos ameambia klabu hiyo kwamba anataka kuondokaHaki miliki ya picha
Kiungo wa kati wa Real Madrid Dani Ceballos ameambia klabu hiyo kwamba anataka kuondoka huku Liverpool ikidaiwa kuwa na hamu ya kumsajili raia huyo wa Uhispania mwenye umri wa miaka 21. (Diario Gol - in Spanish)
Hearts wanajiandaa kumsajili beki wa kushoto wa Manchester United Demetri Mitchell kwa mkopo.
Beki huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 20 atakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na klabu hiyo ya Uskochi wakati wa dirisha la uhamisho la mwezi Januari.(Edinburgh Evening News)
Beki wa Barcelona Gerard Pique ameionya Manchester United kwamba beki mwenza Samuel Umtiti atasalia katika klabu hiyo kwa ''miaka mingi ijayo''
Beki wa Barcelona Gerard Pique ameionya Manchester United kwamba beki mwenza Samuel Umtiti atasalia katika klabu hiyo kwa ''miaka mingi ijayo'' .
Mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24 anaweza kuondoka katika klabu hiyo baada ya Barcelona kulipa kitita cha kumwachilia cha £55m mbali na dau la uhamisho huo(Metro)
Wakati huohuo klabu hiyo ya Catalan inakaribia kumsajili beki wa Palmeiras Yerry Mina. Raia huyo wa Colombia ataweka saini ya kandarasi ya miaka mitano na nusu . (Radio Catalunya - in Spanish)
Javier Mascherano
Anatarajiwa kuchukua mahala pake beki wa Barca na Argentina ,33, Javier Mascherano ambaye anatarajiwa kujiunga na klabu ya ligi ya Superleague nchini China Hebei China Fortune. (Goal)
Kiungo wa kati wa Ujerumani na Juventus Sami Khedira, 30, anasema kuwa hayuko tayari kucheza nchini Marekani na anataka kusalia mjini Turin wakati ambapo kandarasi yake itakamilika 2019(Gazzetta dello Sport)
Millwall imewasiliana na Aston Villa kuhusu kumsajili beki mwenye umri wa miaka 30 Tommy Elphick kwa mkopo kwa kipindi cha msimu kilichosalia.
Sami Khedira
Meneja wa Villa Steve Bruce amekataa kuondoa uwezekano wa mchezaji huyo kuondoka klabu hiyo mwezi huu. (Birmingham Mail)
Mkufunzi wa Newcastle Rafael Benitez anatarajiwa kusisitiza ombi lake kwa mmiliki wa klabu hiyo Mike Ashley na mkurugenzi mkuu Lee Charnley kuhakikisha kuwa wachezaji wanasaini kandarasi mpya kabla ya kukamilika kwa muda wa mwisho aliouweka wa tarehe 20 Januari. (Newcastle Chronicle)

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.