Tahadhari ya kombora isiyo ya kweli yasababisha hofu Hawaii Marekani
Tahadhari ya kuja kwa kombora ilisababisha wakaazi wa jimbo la Hwaii kushikwa na hofu siku ya Jumamosi kabla ya tahadhari hiyo kutangazwa kuwa isiyo ya kweli.
Watumiaji wa simu walipokea ujumbe wa simu uliosema: Kombora la masafa marefu linaelekea Hawaii. Tafuta eneo salama. Haya sio mazoezi.
Gavana wa jimbo aliomba msamaha na kuongeza kuwa hilo lilisababishwa na mfanyaakzi aliyebonyeza kionyezo tofauti.
Serikali ya jimbo la Hawaii imekiri kwamba tahadhari iliyotolewa kimakosa kuhusu shambulizi la kombora la masafa marefu iliathiri zaidi ya watu milioni moja baada ya afisa mmoja kubonyeza kitufe kimakosa.
Tahadhari hiyo ilisambaratisha matangazo ya runinga na radio na pia kutuma ujumbe kwenye simu za watu kuwaonya watafute maeneo ya kujikinga dhidi ya shambulizi hilo.
Gavan Ige amesema mikakati imechukuliwa kuhakikisha kosa hilo halitofanyika tena, japo akasema haielweki mbona vingora vingine - vinavyowashwa kwa njia tofauti - vilisikika vikilia.
Hali hiyo ya tahadhari ilisababisha watu wengi kukimbia bila mwelekeo mitaani na madereva kuendesha magari kwa hofu kubwa, huku wengine wakitafuta hifadhi kwenye maeneo tofauti katika jimbo hilo.
No comments