Ads

RT yashtukia kitu mchongo wa Madola


By IMANI MAKONGORO
KUMEKUCHA. Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) limeshtuka na kuanza kukinukisha ikiwa ni siku 88 kabla ya kuanza kwa Michezo ya Madola itakayofanyikia Australia.
Vigogo wa RT wameeleza wameanza kuhisi dalili mbaya wanazoweza kufanyiwa wanariadha wao waliofuzu kushiriki michezo hiyo itakayochezwa kati ya Aprili 5-14.
Kama haitoshi, vigogo hao walichimba mkwara kamwe hawatakubali kuja kuona kile walichokishtukia sasa kinakuja kuwa kweli wakati msafara wa timu ya Tanzania utakapotakiwa kwenda kwenye Mji wa Christ Church tayari kwa michezo hiyo.
“Wanariadha wetu waliokwishafuzu ni 10, lakini kuna dalili tulizoshtukia za kutaka waombewe visa wachache, eti nusu yao hilo hatuwezi kulikubali,” alisema Katibu Mkuu wa RT, Wilhelim Gidabuday.
“Tunachokitaka ni wanariadha wote waliofuzu waombewe visa, ikitokea tumeshindwa kuwapeleka wote, basi RT tuchague yupi aende na yupi abaki, lakini kuanza kuwabagua mapema katika kuwaombea visa hilo suala tusilokubaliana nao.
“Tutakwenda kwa Mkurugenzi wa Michezo (Yusuf Singo), yeye ndiye Mkuu wa msafara Australia kumueleza hili, isije kufikia mwishoni aliyeombewa visa kaumia na ambaye yuko fiti hana visa, tunataka waombewe wote 10,” alisema Gidabuday.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.