Marekani yapunguza makali kwa Wakimbizi
Maafisa nchini Marekani wamesema marufuku iliyopigwa juu ya Wakimbizi kutoka nchi 11, iliyokuwa ikichukuliwa kuwa ni hatari sasa imeondolewa. Hata hivyo watachunguzwa kwa umakini.
Waziri wa Usalama wa Ndani nchini humo Kirstjen Nielsen amesema tathmini ya hatari itachukuliwa kwa kila mkimbizi kabla ya kumkubalia kuingia nchini humo.
Oktoba mwaka jana, Utawala wa Rais Donald Trump ulipiga marufuku wakimbizi kutoka mataifa 10 yenye asilimia kubwa ya Waislamu na wa kutoka Korea Kaskazini.
Ni wakimbizi 23 tu kutoka katika nchi hizo ndio wameweza kuingia Marekani toka wakati huo, baada ya Jaji nchini humo kwa kiasi fulani kuweza kuizuia amri hiyo iliyotolewa na serikali.
No comments