Daktari wa timu ya Olimpiki Marekani ahukumiwa kifungo
Aliyekuwa daktari wa timu ya Olimpik Larry Nasser amehukumiwa kwenda jela miaka 175 baada ya kukutwa na makosa ya ukatili wa kingono dhidi wananawake na wana michezo.
Katika kesi hiyo mashahidi 160 wamewasilisha ushahidi wao huku Nasser mwenyewe alikiri makosa kumi, japo kuwa hata hivyo alikuwa akitumikia kifungo cha miaka 60 kutokana kutokana kukutwa na hatia ya kumiliki picha ngono za watoto kinyume cha sheria.
Jaji Rosemary Aquilina ameiambia mahakama kuwa amejisikia fahari na furaha kubwa kutoa adhabu hiyo kutokana na kitendo alichofanya Nasser na kwamba anataka iwe fundisho kwa wengine.
'Nataka ukae jela maisha yako yote'. Hata hivyo baada ya hukumu hiyo mmoja wa waathirika amesisitiza kuwa washirika wa daktari huyo wanapaswa kushitakiwa pia.
Hukumu ya Larry Naser inafuatia wiki ya ushuhuda kutoka kwa wanawake takribani mia moja na sitini, wakiwemo washindi wa medali ya dhahabu ya olympiki Biles, Aly Raisman, Gabby Douglas na McKayla Maroney
No comments