Hii hapa mikoa minne iliyoteuliwa na tff kwaajili ya Michuano Ya U 17 Ya Afcon 2019
Kazi imeanza. Mikoa ya Arusha, Mwanza, Dodoma na Dar es Salaam ndiyo inapigiwa hesabu ya viwanja vyake kutumika kwenye mashindano ya Mataifa ya Afrika ya Vijana (AFCON).
Tanzania itakuwa mwenyeji wa mashindano hayo ya 2019 na tayari Serikali imekubali uenyeji huo na jana Jumamosi Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe alizindua kamati ya kitaifa ya mashindano hayo.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Nchini, Yusufu Singo alisema; "Tunategemea kuwapokea wataalamu kutoka CAF wakati wowote kuanzia sasa maana tumeambiwa watawasili nchini haraka iwezekananvyo, huenda ikawa mwezi huu wa Novemba, pamoja na mambo mengine lakini kikubwa wanachokuja kukifanya ni ukaguzi wa viwanja vitakavyotumika.
"Tunategemea kuwapeleka katika mikoa ya Mwanza, Arusha, Dodoma na Dar es Salaam kisha wao sasa ndiyo watashauri ni viwanja vipi ambavyo wanaona vinastahili kutumika kwenye AFCON na vitu gani vya kuboreshwa zaidi," alisema Singo.
No comments