TRUMP KUJITOA KWENYE MKATABA NA IRAN
Rais wa Marekani Donald Trump ameupuuzilia mbali mapatano ya kinyukilia na Iran na kutisha kuwa atajiondoa katika mkataba wa kimataifa unaohusiana na nyuklia iwapo bunge la Congress litakosa kuidhinisha mapendekezo yake.
Alitoa tangazo hilo kama sehemu moja ya kubadilisha msimamo kuhusiana na Iran ili Marekani iweze kuchukua hatua kali zaidi dhidi ya Iran kuhusiana na uimarishaji wake wa makombora ya kisasa na uungaji wake mkono kwa makundi ya kigaidi katika mashariki ya kati.
Rais Trump amesema kuwa uongozi wa Marekani dhidi ya Iran ni ule wa kukabiliana na taifa sugu linalounga mkono ugaidi na si muhimu kuwa na mkataba ambao lengo lake ni kuzuia taifa hilo la Kiarabu kuimarisha zana zake za kinukilia.
Alishutumu mapatano hayo kama hafifu na akakataa kuthibitisha iwapo Marekani inanufaika vyovyote kutokana nao.
Alisema kuwa Bunge la Congress linapaswa kuchukua hatua kurekebisha hali hiyo.
Kwa sasa wanachama wengi wa Congress hawana moyo wa kutaka kufutilia mbali mkataba huo, badala yake wanasema kuwa wako tayari kushirikiana na Bwana Trump kuufanyia ukarabati.
Mataifa ya Ulaya yamesema kuwa sio wajibu wa Marekani kuufanyia marekebisho mkataba huo kwa sababu utengenezaji wake ulishirikisha mataifa mengine matano na kuidhinishwa na Umoja wa Mataifa.
Ulaya inasema kuwa Bunge la Congress linapaswa kufikiria kwa undani matokeo ya usalama ya hatua yoyote kuhusiana na mapatano hayo kabla ya kufanya marekebisho.
Iran imesema kuwa haina nia ya kufanya mashauriano mapya wala kushinikizwa na mataifa yoyote ya kigeni.
Hatahivyo Rais Trump amesema kuwa anakusudia kuimarisha vikwazo dhidi ya Iran huku akisisitiza kwamba atatilia kipao mbele kikosi maalumu cha kijeshi nchini humo kijulikanacho kama Revolutionary Guards
No comments