Ads

BREAKING NEWS, Serikali ya kenya yapiga marufuku maandamano



Image result for breaking news

Serikali nchini Kenya imepiga marufuku maandamano katika maeneo ya katikati mwa miji ya Nairobi, Mombasa na Kisumu.
Kaimu waziri wa usalama Dkt Fred Matiang'i amesema pia kwamba wanaopanga maandamano wanafaa kuwajibishwa kutokana na uharibifu wa mali unaotokea wakati wa maandamano.
Hatua ya Dkt Matiang'i imetokea huku muungano wa upinzani National Super Alliance (Nasa) wake Raila Odinga ukiendelea na maandamano ya kushinikiza mageuzi katika Tume ya Uchaguzi (IEBC). 
Jumatano, visa vya uporaji wa mali viliripotiwa katikati mwa jiji la Nairobi.
Mmoja wa viongozi wa Nasa James Orengo, ambaye alikuwa naibu ajenti mkuu wa Bw Odinga wakati wa uchaguzi wa mwezi Agosti ambao ulifutiliwa mbali na Mahakama ya Juu, alitoa wito kwa wafuasi wa muungano huo kuandamana kila siku.

VIDEO WAZIRI MKUCHIKA AKABIDHIWA OFISI RASMI

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.